Home Uncategorized PAPY TSHISHIMBI ABAKIZA SIKU MBILI NDANI YA YANGA, VIONGOZI WASIMULIA NAMNA WANAVYOPAMBANA

PAPY TSHISHIMBI ABAKIZA SIKU MBILI NDANI YA YANGA, VIONGOZI WASIMULIA NAMNA WANAVYOPAMBANA


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa nahodha wao Papy Tshishimbi mkataba wake unafika ukingoni mwezi Agosti ambapo kwa sasa zimebaki siku mbili sawa na saa 48 ili awe mchezaji huru, hivyo jitihada zinafanyika ili kumuongezea mkataba kiungo huyo mkabaji.
Tshishimbi amekuwa kwenye mvutano mkubwa na uongozi kuhusu mkataba wake, mara ya mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa Julai 12, mwaka huu pale Uwanja wa Taifa kwenye dabi wakati Yanga ikipoteza kwa kufungwa mabao 4-1 mbele ya Simba kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.
Akizungumza na Championi Jumatano, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa nyota huyo hajasaini kwenye timu nyingine kama inavyodaiwa.

“Tshishimbi ana mkataba na Yanga kwa sasa ukiwa unakaribia kuisha mwezi Agosti, mkataba wake utakuwa umefika tamati ila kwa sasa tupo kwenye mazungumzo naye kwani ni mchezaji mzuri na kazi yake anatimiza ndani ya uwanja.
“Kila siku tunawasiliana naye ili kufika kwenye makubaliano kwani mchezaji hawezi kusaini ikiwa hajakubali nasi pia tunamskiliza ili tujue anahitaji nini, ninaamini atakuwa ndani ya Yanga kwani hatutashindwana naye,” alisema Mwakalebela.

Msimu wa 2019/20, Tshishimbi amekuwa akitajwa kuibukia kwa watani wao, Simba kwa ajili ya kuongeza nguvu kikosini hapo kwa msimu wa 2020/21.
SOMA NA HII  HAWA NDIO ANGUKO LA GAMONDI