Home Habari za michezo MANARA – FEI TOTO ANAIHUJUMU YANGA….HATUTAMPA MEDALI YA CAF….

MANARA – FEI TOTO ANAIHUJUMU YANGA….HATUTAMPA MEDALI YA CAF….

Tetesi za Usajili Yanga

Aliyekuwa msemaji wa Yanga, Haji Manara amemtolea uvivu Feisal Salum baada ya kiungo huyo wa Yanga SC kuomba kuchangiwa pesa kwa ajili ya kulipia gharama za kufungua jalada la kesi kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS)

Ni aibu kubwa kwa Nchi ni fadhaa na kulikosea Taifa hili, Kwa mara nyingine tena Fesal Salum anashiriki kuihujumu Yanga Waziwazi bila haya.

Tupo karibu kabisa na finali kubwa mbele yetu,Rais Wa Nchi yupo busy mara kwa mara kuhamasisha watanzania, Bunge kupitia Waziri Mkuu wanahamasisha, Wakuu wa mikoa ndio kama mnavyosikia.

Kisha anatokea Binadamu anaepotoshwa na Watu wale wale kila tunapokaribia mechi kubwa kutuletea mjadala wa jambo lake binafsi lisilokuwa na chembe ya maslahi ya Taifa kutuletea choko choko.

Hivi hii sio hujuma ya kusudi kwetu na kwa nchi? Mawakili wake,Mameneja wake na hata Radio zinazopush agenda yake kipindi hiki tukisema wanatuhujumu kusudi tutakuwa tunakosea?

Kwanza anachangisha nini wakati majuzi tu kaleta Milioni Mia ya kuvunja mkataba? Kwa nn asichukue ile Vits Ya Dalali wake akauza ili aende CAS?

Fesal unaendelea kutengeneza ufa ndani ya mioyo ya wengi, Yanga hii unayotafuta huruma mitandaoni ndio iliyokulea na kukupa jina unalosafiria nalo hivi sasa, Yanga hii hii ndio ilipokufanya uwe na hilo jina ambalo hao wanaokudanganya leo walikujulia hapa.

Mbaya zaid Mchambuzi mpumbav yule yule toka Radio ile ile yupo front kuendelea kukupotosha, Taifa linasulubiwa kwa sababu yako Fei, Nchi ipo katika vita ya ubingwa,wew unashiriki vita yako ya huruma za kinafik.

Unasema eti mama yako alitukanwa, yy na Yanga nani kamtusi mwenzie? Kutwambia ulikuwa unakula Ugali na Sukari sio matusi na dhihaka kwetu,

Ni kweli mara nyingi umekuwa unatufanyia hv kila tunapokaribia mechi kubwa, lakini kwa mechi hii nathubutu kumwambia wazi wazi ww ni Mhujumu unaetumika bila kujijua,Ww ni Msaliti, Ww sio Muungwana hata chembe, unaihujumu Yanga.

Why usisubiri mechi iishe? Why iwe leo? Na kwa nn kila mechi yetu kubwa unarudia drama zako?

Tushinde tushindwe hupati hata medali moja, mjinga sana ww Mtoto, unafanya hvyo kwa maslahi gani? Yanga imekukosea nn cha Ziada hadi uwe unatufanyia hvyo na huyo Shankupe wako muuza na nywele za maiti?

SOMA NA HII  CHAMA AWEKA REKODI YA KIBABE NYUMBANI