Home Habari za michezo MGUNDA:- KAMA MATUSI YA KAMWE NI ILI YANGA ISHINDE BASI SAWA…ILA WASIPOSHINDA...

MGUNDA:- KAMA MATUSI YA KAMWE NI ILI YANGA ISHINDE BASI SAWA…ILA WASIPOSHINDA KESHO….

Habari za michezo bongo

Kocha Msaidizi wa Simba SC Juma Ramadhan Mgunda amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kutupiwa maneno ya kashfa na Afisa Habari wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Ally Kamwe.

Kashfa za Kamwe zilisikika wakati wa Hamasa ya Young Africans iliyofanyika jana Ijumaa (Mei 26) katika Viwanja vya Zakhiem-Mbagala jijini Dar es salaam, kuelekea mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Ally Kamwe alisema Andazi ni bora kuliko Kocha Mgunda, ambaye amekuwa sehemu ya Benchi la Ufundi la Simba SC tangu mwanzoni mwa msimu huu, baada ya kuondoka kwa Kocha Zoran Maki.

Akijibu dhihaka na maneno hayo ya kashfa dhidi yake Juma Mgunda amesema: “Sijui kinachopelekea mimi kuwa miongoni mwa kampeni hii ya matusi na kunidhalilisha nilidhani kampeni itakuwa ni kushinda fainali, kuliko hiki alichokifanya Mwanangu Ally Kamwe.

“Kama nilipaswa kutukanwa ili Yanga ishinde basi nimekubali ili Taifa langu lijivunie.

“Tusiposhinda kesho nitashangaa sana kwa nini tumefungwa wakati kilichotakiwa kifanywe kimefanywa juu yangu na familia yangu” Kocha Juma Mgunda.

“Namuombea kwa Mungu awe na mwisho mzuri , mimi nimeshuhudia watu wengi wakifanya kazi Yanga na Simba na sasa wapo nje ya mfumo.

“Yanga ni Klabu yetu pekee Tanzania inayotuwakilisha kwenye fainaly hii ya CAF na kwa bahati iliyonjema inacheza na Club Inayotoka nje ya nchi yetu,” amesema Mgunda.

SOMA NA HII  YANGA WAIBUKA NA 'MIHOGO PARTY'....ALLY KAMWE AFUNGUKA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI...

1 COMMENT

  1. Huyu kijana kamwe hana heshima kabisa alicho kifanya ni kuwa haribia vijana wenzake uaminifu wakupewa wadhifa mkubwa kama uo alipewa yeye na yanga maana yanga haikumtuma aende kuwa kashifu wazee kama nisawa mbona asimfananishe baba ake mzazi na andazi ajue hiyo mgunda ana watotio Tena wenye heshima zao hapa Tanga yanga twaipenda sana twaomba imuondoe kabisa kataka wadhifa huo ili iwe fundisho kwa vina wengine wasio kua na heshima na wazee kama yeye