Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA BALEKE KUSEPA SIMBA SC….WAKALA WAKE AVUNJA UKIMYA…AANIKA MIPANGO YA...

KUHUSU ISHU YA BALEKE KUSEPA SIMBA SC….WAKALA WAKE AVUNJA UKIMYA…AANIKA MIPANGO YA MAZEMBE…

Habari za Simba SC

Wakala wa Jean Baleke athibitisha kuwa; hafikirii mchezaji huyo atabaki Simba SC zaidi ya mkataba wake wa mkopo.

Alisema: “Sidhani kama atabaki Simba. Aidha TP Mazembe itajaribu kumrudisha au kumuuza. Huu ndio ukweli

Aliongeza kuwa vilabu kutoka Asia na Ulaya vimeanza kufanya mawasiliano.

Bakeke alijiunga Simba kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Disemba mwaka jana ambapo toka ajiunge amekuwa na msaada mkubwa kwa upande wa Wekundu hao wa Msimbazi.

Miongoni mwa “Impact” zake klabuni hapo ni pamoja na kuifungia timu kwenye mechi muhimu huku pia akitumia magoli matatu kwenye mechi dhidi ya Mtibwa.

Magoli mengine amefunga kwenye mechi za kombe la FA pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika .

Hata hivyo inaelezwa kuwa Simba wanafanya kila jitihada kuhakikisha wanambakisha nyota huyo ambaye ametokea kuzikonga nyoyo za mashabiki wa soka nchini.

Chanzo: MickyJr

SOMA NA HII  TATIZO LA SIMBA MSIMU HUU HILI HAPA....WAKISHINDA KUTATUA WATALIA SANA TU....