Home Azam FC ‘SOPU’ AJILENGESHA TENA KWA MADAKA MISHALE WA YANGA…AFUNGUKA ANAVYOMUOTEAGA..

‘SOPU’ AJILENGESHA TENA KWA MADAKA MISHALE WA YANGA…AFUNGUKA ANAVYOMUOTEAGA..

Habari za Michezo

Mshambuliaji wa Azam FC, Abdul Suleiman ‘Sopu’, amesema anatamani Yanga ishinde mchezo wa Nusu Fainali wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC), ili akakutane tena na kipa Djigui Diarra kwenye mechi ya fainali.

Akizungumza nasi, mshambuliaji huyo amesema anajua udhaifu wa kipa huyo ndio maana anatamani kukutana naye, ili aisaidie timu yake kubeba ubingwa.

“Diarra ni kipa mzuri lakini huwa sipati tabu kumfunga, najua upungufu wake na ndio huwa natumia kumfunga mara kwa mara,” amesema Sopu na kueleza kuwa anataka wakutane naye ili amfunge tena.

Katika mchezo wa Fainali ya Kombe la ASFC msimu uliopita kati ya Coastal Union na Yanga, Sopu alifunga hat-trick katika sare ya mabao 3-3, kabla ya Yanga kushinda Kwa mikwaju ya penalti.

Mchezo wa marudiano Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, kati ya Yanga na Azam, ambao Yanga ilishinda mabao 3-2, mabao ya Azam yalifungwa na Sopu.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO.....AHMED ALLY AFUNGUKA ISHU YA JOHN BOCCO NA HOFU ILIYOKUWEPO...ATOA OMBI...