Wakati Yanga jana walikuwa dimbani kupambania heshima yao kwenye soka la Afrika , japo mambo hayakwenda sawa, Rais wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA, Gianni Infantino amewatumia salamu za pongezi.
Gianni ambaye amekuwa na kawaida ya kuipongeza timu/klabu zinazofanya vizuri sehemu mbalimbali duniani, ametuma ujumbe huo kwa Yanga kupitia Shirikisho la Soka nchini TFF.
Katika Ujumbe huo, Infantinho amenukuliwa akiipongeza Yanga kwa namna walivyopambana kuupata ubingwa wa Tanzania, huku pongezi zake hizo zikienda mbali zaidi kwa viongozi na watu wote waliohusika.
JUHUDI, bidii, ari ya kujitolea imetajwa kuwa miongoni mwa sababu zilizowapa Yanga ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/2023.
Rais wa FIFA, Gianni Infantino amesema hayo kupitia barua iliyotolewa leo na Shirikisho la Soka (TFF).
Katika taarifa hiyo Infantino ameipongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa huo sambamba na waliohusika katika safari hiyo ya mafanikio.
Rais huyo ameipongeza pia TFF kwa mchango wake katika maendeleo na ustawi wa soka la Tanzania na Afrika.
Itakumbukwa kuwa Yanga wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu, huku wakiwa na michezo miwili mkononi, pamoja na kufika Fainal ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo jana walipata ushindi mdogo ambao haukuweza kupata taji hilo.
Pamoja na mafaniko hayo, Pia Yanga imetinga faina ya Kombe la Shirikisho la TFF maarufu kama ASFC ambapo watacheza na Azam FC baadaye mwezi huu mkoani Tanga.