Home Habari za michezo BOCCO ASHINDANIDHWA NA KIGOGO HUYU UMENEJA WA SIMBA….MSIMAMO WAKE HUU HAPA..

BOCCO ASHINDANIDHWA NA KIGOGO HUYU UMENEJA WA SIMBA….MSIMAMO WAKE HUU HAPA..

Habari za Simba SC

Jina la nahodha wa Simba, John Bocco ni kati ya majina mawili yaliyopendekezwa kumrithi aliyekuwa Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu ambaye amepewe majukumu mengine kwenye upande wa timu za vijana.

Jina la Bocco na mratibu wa timu hiyo Abbas Suleiman ndio wanatajwa huku mabosi wa Simba wanataka Bocco ndiye awe Meneja kutokana na ushawishi alionao na ukaribu kwa wachezaji baada ya kuwaongoza kwa muda mrefu kama nahodha wao.

Hata hivyo mbali na mvutano wa pande mbili juu ya jina la Bocco, inadaiwa nyota huyo bado anataka kucheza soka akiamini ana uwezo mkubwa wa kuendelea kufumania nyavu.

Hii inakuja baada ya hivi karibuni, Simba kumpa majukumu mengine Patrick Rweyemamu ambapo sasa atakuwa ni Mkuu wa Idara ya timu za vijana ndani ya klabu hiyo.

Aidha kwa upande mwingine, Abbasi yeye ni mratibu wa timu hiyo, ambapo amekuwa akihudumu kwenye kuhakiksha safari za timu hiyo ndani na nnje ya nchi zinakuwa kwenye mpangilio wake.

Hata hivyo, huenda ikawa ni ngumu kwa wote hao kupewa nafasi hiyo haswa ukizingatia wawili hao wanamajukumu mengine ya kimsingi ndani ya timu hiyo.

SOMA NA HII  PETER BANDA AITWA TIMU YA TAIFA YA MALAWI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here