Home Habari za michezo KUHUSU TUHUMA ZA KUUZA MECHI YANGA…FEI TOTO AIBUKA NA HILI JIPYA…AKUMBUSHIA YA...

KUHUSU TUHUMA ZA KUUZA MECHI YANGA…FEI TOTO AIBUKA NA HILI JIPYA…AKUMBUSHIA YA MAMA YAKE..

Habari za Yanga

Kiungo wa Yanga SC, Feisal Salum (Fei Toto) amesema alifikia uamuzi wa kuvunja mkataba na klabu hiyo kutokana na manyanyaso aliyokuwa akiyapata kutoka kwa uongozi, ikiwemo kuzushiwa kwamba ameuza mechi.

Akizungumza kupitia Clouds FM, Fei Toto amesema tangu aliposaini mkataba mpya na Yanga ambao unaisha mwakani, manyanyaso ndio yamezidi na kwamba ada yake ya uhamisho ilikuwa shida na kwamba mshahara analipwa lakini kwa manyanyaso.

“Mimi nimeshalia uwanjani… kiongozi anakutukana ‘kama huwezi utarudi kwenu Pemba… lakini nikaendelea kuvumilia,” amesema Fei.

Ameongeza kuwa manyanyaso hayo hayakuishia kwake bali yalikwenda hadi kwa mama yake mzazi ikiwemo kumtusi kwa kumuita “Andazi,” na kwamba Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said anawaaminisha watu kwamba Fei Toto ni mbaya.

SOMA NA HII  NABI AWAPONGEZA WACHEZAJI WAKE KWA USHINDI

1 COMMENT

  1. Sio vyema kwa wanavyokua wakiwafanyia wachezaji hivi kama fei anasema ukweli