Home news KIMEUMANA..GOMES ASHINDWA KUVUMILIA TABIA ZA MORISSON NA MKUDE..MSENEGALI NAYE YUMO..

KIMEUMANA..GOMES ASHINDWA KUVUMILIA TABIA ZA MORISSON NA MKUDE..MSENEGALI NAYE YUMO..


UNAAMBIWA! Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes Da Rosa, amewataka nyota wake wote waliopo kwenye mapumziko mafupi kutojisahau kufanya mazoezi binafsi wakiwemo Ousmane Sakho na Bernard Morrison, huku akisema atakayerejea mazoezini hana utimamu wa mwili atakiona cha moto.

Gomes alitoa mapumziko ya siku 10, kwa nyota wake baada ya kikosi hicho kurejea kutoka katika kambi yao ya maandalizi iliyokuwa nchini Morocco kwa wiki mbili.Timu hiyo ipo mapumzikoni kupisha michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Qatar.

Mmoja wa mabosi kutoka Benchi la Ufundi la timu hiyo, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, Gomes amewataka wachezaji wake ambao hawapo katika majukumu ya timu ya taifa, kuendelea kufanya mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kujiweka fiti.

Bosi huyo alisema kuwa hataki kuona mchezaji yeyote akiongezeka uzito mara baada ya timu itakaporejea kuendelea na mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya ‘pre-seasson’.Aliongeza kuwa kocha huyo amepanga kuwapima uzito wachezaji wote kikosi hicho kitakaporejea kambini kuendelea na mazoezi.

“Kocha baada ya kuwapa mapumziko wachezaji ambao hawapo katika timu za taifa, haraka akaagiza kuwa kila mchezaji ahakikishe anafanya mazoezi ya kutosha ili mara atakaporejea kambini asije kuanza moja tena kutafuta utimamu wa mwili.

“Na hili alilikazia kwa Morrison, Mkude (Jonas) na wachezaji wapya waliosajiliwa katika kuelekea msimu ujao.“Kocha alisisitiza zaidi kwa hao kwa sababu anawajua wachezaji hao wana tabia za kula bata sana na mara kadhaa wanajikuta hata hawapati muda wa mazoezi nje ya timu, jambo ambalo kocha hataki kuona linatokea,” kilisema chanzo hicho.

Meneja Mkuu wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu juzi aliliambia gazeti hili kwa kusema kuwa:

“Benchi la Ufundi limepanga kukutana ndani ya siku hizi mbili kwa ajili ya kupanga siku ya kuanza na program za mazoezi.”

SOMA NA HII  GAMONDI:- SIMBA INA UBORA WAKE.....YANGA HAIJAKAMILIKA...KUNA MAPUNGUFU MENGI...