Home Habari za michezo PAMOJA NA YANGA KUTOKA KAPA JANA….HIVI NDIVYO ‘SURE BOY’ ALIVYOKICHAFUA PALE KATI...

PAMOJA NA YANGA KUTOKA KAPA JANA….HIVI NDIVYO ‘SURE BOY’ ALIVYOKICHAFUA PALE KATI MBELE YA WAARABU..

Habari za Yanga

Jana wakati Yanga wakitetea heshima ya nchi, nchini Algeria, moja kati ya wachezaji waliotakata ukiacha wengine ni pamoja na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Sure Boy ambaye alicheza mwanzo mwisho, alifanikiwa kung’aa na kuiwezesha Yanga haswa sehemu ya kiungo kutulia kwa muda wote wa mchezo.

Sure Boy alisimama sambamba na Mudathir Yahaya ambaye mara kadhaa naye alihusika kwenye mijongea ya kuisogeza timu mbele.

Hata hivyo haikuwa safari nyepesi sana kwa Sure Boy ambaye jana ilimbidi Kocha Nabi Kufunga mwacho na kumwanzisha hukua akimweka benchi kiungo mkata shombo Litombo Bangala nnje.

Kutoka Viungo vya Chamazi mpaka mitaa ya twiga na Jangwani medali mbili za ligi kuu medali moja ya kombe la shirikisho la Azam Sports federation Cup medali moja ya ngao ya jamii .

Jana amevaa medali ya ushindi wa pili wa kombe la shirikisho barani Afrika . Hapo akiwa na msimu mmoja na Nusu na kikosi cha Wananchi jina la Sure boy amerithi kutoka kwa baba yake ambaye pia alikuwa mchezaji wa wananchi Yanga.

Jana alipiga pasi 55 kati ya hizo pasi 41 ndio zilifanikiwa kufika lakini ndio mchezaji aliyepiga pasi nyingi kwa timu zote mbili. Katika pasi 328 walizo piga Yanga jana basi 55 zilipigwa na Sure boy .

Ukimtoa Sure boy wanao fata kwa kupiga pasi nyingi ni kipa wa Yanga Djigui Diarra pasi 39 zikifika pasi 29 na Beki Ibrahim Bacca pasi pasi 48 zikifika pasi 28.

Jana Yanga walikuwa dimbani nchini Algeria kukipiga na USMA ambapo mbali na kuibuka na ushindi wa goli 1-0 walishindwa kubeba ubingwa kutokana na USMA kuwa na mtaji mkubwa wa magoli ya nyumbani.

SOMA NA HII  MASTAA YANGA WAZIDI KUISHIKA CAF KILA KONA ....SIMBA MHHHH...