Home Habari za michezo BANGALA NA DJUMA WAPIGWA PINI YANGA…ISHU YAO YA KWENDA SIMBA YAFIA MEZANI…

BANGALA NA DJUMA WAPIGWA PINI YANGA…ISHU YAO YA KWENDA SIMBA YAFIA MEZANI…

Habari za Yanga leo

Kabla mabosi wa Young Africans hawajakutana juma hili na wachezaji wa timu hiyo, Djuma Shaban na Yannick Bangala, Wakongomani hao walikinukisha wakishinikiza kuondoka.

Nyota hao ambao bado wana mkataba na Young Africans hadi 2024, walikuwa wakishinikiza kuondoka, lakini baada ya kufanyika kikao kizito, wamekubali kubaki kutokana na masharti mazito waliyopewa.

Mmoja wa mabosi wa timu hiyo, amesema kuwa, wachezaji hao katika kikao hicho wameruhusiwa kuondoka Young Africans kwa sharti la kusajiliwa na klabu nyingine ya hapa nchini tofauti na Simba SC na Azam FC.

Bosi huyo amesema kuwa, katika kikao hicho wachezaji hao waligomea sharti hilo, huku wakishinikiza kuondoka kwenda wanapopahitaji, lakini baada ya kukaziwa na uongozi, wakabadili uamuzi na kufikia muafaka wa kukubali kumalizia mkataba wa mwaka mmoja waliobakisha unaomalizika 2024.

Ameongeza kuwa, Bangala na Djuma wameahidi kutoa ushirikiano kwa Kocha mpya Muargentina, Miguel Angel Gamondi na wachezaji wenzao katika kuelekea msimu ujao.

“Kikao kizito kilifanywa jana (juzi) Jumanne kati ya uongozi na wachezaji Bangala na Djuma ambacho kimefikia muafaka mzuri wa pande mbili kuendelea kufanya kazi pamoja kumalizia sehemu ya mikataba yao itakayomalizika 2024.

“Katika kikao hicho, mengi yalizungumzwa ikiwemo wachezaji hao kuomba kuvunjiwa mikataba yao, kitu ambacho uongozi uliridhia kuwaruhusu kuondoka kwa sharti la kusajiliwa na timu ndogo za ndani, lakini zisiwe Simba SC na Azam FC.

“Sharti hilo lilikuwa gumu kwao na kukubali kumalizia mkataba wao wa mwaka mmoja baada ya hapo waondoke zao, wachezaji hao wameonekana kuwa wasumbufu kwa uongozi kila wakati, hivyo wamekubaliana kwa pamoja kufikia maamuzi hayo ya kumalizia muda huo walioubakisha,” amesema bosi huyo.

Bangala baada ya kikao hicho, aliandika ujumbe mzito kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii uliosomeka hivi: “Napenda kuwashukuru mashabiki wote wa Young Africans kwa sababu siku chache zilizopita mmeandika mengi kuhusu hali yangu klabuni, kama unavyojua nina mkataba na klabu hadi 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here