Home Azam FC BAADA YA KUILIZA YANGA KWA FEI TOTO….SASA ZAMU YA SIMBA…MABOSI AZAM WAAPA...

BAADA YA KUILIZA YANGA KWA FEI TOTO….SASA ZAMU YA SIMBA…MABOSI AZAM WAAPA KUMBEBA STAA HUYU..

Habari za Simba SC

Baada ya kumalizana na Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ akitokea Young Africans, Uongozi wa Azam FC unatajwa kuhamishia nguvu Simba SC ukijipanga kumsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Malawi Peter Banda.

Taarifa zinaeleza kuwa Azam FC imeanza mazungumzo na wawakilishi wa nyota huyo wa kimataifa wa Malawi mwenye miaka 22.

Inaelezwa kwamba kwa hatua waliyofikia kuna uwezekano mkubwa Banda akavaa uzi wa Azam FC msimu ujao kutokana na Simba SC kuwa tayari kumuuza au kumtoa kwa mkopo kipindi hiki akiwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja.

Nyota huyo tegemeo wa timu ya taifa ya Malawi hayupo kwenye mipango ya kocha mkuu, Roberto Oliveira Robertinho’ aliyowapa mabosi wa chama hilo na Azam inatumia mwanya huo ili kumshawishi atue Chamazi yalipo maskani yao.

Mmoja wa viongozi wa juu wa Azam FC mesema: “Pale Simba tutang’oa mtu kama tulivyowapa wao wachezaji miaka ya nyuma na sisi watatupa mastaa wao mmoja wao ni yule winga Banda. Kama wanaona hawafai, sisi atatufaa na tunajua tutamtumiaje” amesema mtu huyo.

Banda alisajiliwa Simba SC mwanzo a msimu uliopita akitokea Nyassa Big Bullets ya Malawi, lakini tangu ametua hana mwendelezo huku majeraha ya mara kwa mara yakitajwa kumtesa Juhudi za kumpata Banda kuzungumzia suala hilo wala viongozi wa Simba jana harikuzaa matunda.

SOMA NA HII  SAA CHACHE KABLA YA MECHI YA NGAO YA JAMII...STAA WA SIMBA AFUNGUKA A-Z ANAVYOWAGOPA FEI TOTO NA AZIZ KI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here