Home Habari za michezo KUHUSU KUWEKA KAMBI YAO UTURUKI…SIMBA WAIBUKA NA HILI JIPYA…

KUHUSU KUWEKA KAMBI YAO UTURUKI…SIMBA WAIBUKA NA HILI JIPYA…

Habari za Simba

Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kucheza michezo mitatu ya kirafiki ya Kimataifa ya kujipima nguvu nchini Uturuki, kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Simba SC itakayoondoka juma lijalo, itaweka kambi ya majuma matatu ya kujiweka sawa kabla ya kurejea nchini kuendelea na Programu za msimu mpya 2023/24.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kikosi chao kitaondoka kikiwa na wachezaji wote waliosajiliwa katika kipindi hiki, maafisa wa Benchi la Ufundi na baadhi ya viongozi.

Ally amesema maandalizi ya kambi yamekamilika na wachezaji wapya waliosajiliwa wa ndani, kimataifa watakuwa sehemu ya kambi.

“Kambi Uturuki ni ya mapendekezo ya Kocha Roberto Oliviera Robertinho, amesema anaamini timu ikiwa Uturuki itapata utulivu, wachezaji watapata muda wa kuelewana na kupanga mikakati mbalimbali ya kufanya vyema msimu ujao,” amesema Ahmed.

Pamoja na kambi, ofisa huyo amesema Simba SC inatarajia kuanza kufanya utambulisho wa wachezaji watakaokuwa kikosini msimu ujao.

“Muda wowote kuanzia sasa wachezaji wetu watatambulishwa, jezi zipo tayari na kila kitu kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao kinakwenda vizuri,”ameongeza.

Juzi Jumatatu (Julai 03), baadhi ya wachezaji wa timu hiyo walifanyiwa vipimo vya afya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Daktari wa timu, Edwin Kagabo, alisema wachezaji wamepimwa afya na wote wapo fiti asilimia 100.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO BENCHIKHA ANAVYOPITA 'NYAYO KWA NYAYO' KWENYE NJIA ZA NABI...