Home Habari za michezo STAA MPYA YANGA AWEKA REKODI YA KIBABE TZ…KUMBE ALIKUWA MCHEZA DANSA…

STAA MPYA YANGA AWEKA REKODI YA KIBABE TZ…KUMBE ALIKUWA MCHEZA DANSA…

Habari za Yanga

Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ ameweka rekodi kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika Kusini kucheza ligi kuu ya Tanzania Bara

Kwa lugha nyingine Yanga inakuwa klabu ya kwanza Tanzania kusajili mchezaji wa ligi kuu ya Afrika Kusini

Ubora na thamani ya ligi ya Afrika Kusini ni kubwa kuliko ligi yetu, Skudu anakwenda kufungua milango kwa wachezaji wengine kutoka Afrika Kusini kuja kucheza Tanzania

Skudu ni mchezaji wa daraja la juu, ni aina ya kiungo mshambuliaji/winga ambaye anaweza kufungua mabeki wagumu

Kama Bernard Morrison alijizolea sifa kwa aina yake ya uchezaji ukiondoa changamoto zake za nje ya uwanja, basi mwalimu wake ni Skudu

Skudu ni mchezaji ambaye hahitaji maneno mengi kumuelezea, wale wenye mashaka nae waweke akiba ya maneno, wamsubiri uwanjani

ALIKUWA MCHEZA DANSA.

Winga mpya wa Yanga, Mahlatse Makudubela Manoka ‘Skudu’ raia wa Afrika Kusini kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa alishawahi kuwa dancer wa muziki nchini kwao ndiyo maana ana uwezo mkubwa wa kucheza.

Skudo aliyekuwa akikipiga Marumo Gallants amesema kuwa ameheshimishwa kupewa jezi hiyo na ni deni kwake kuitendea haki ili kuwafurahisha mashabiki wa Yanga kwa kusaidiana na wachezaji wenzake kuiletea mafanikio zaidi klabu hiyo.

“Nilishawahi kuwa dancer, na soka lina vitu vingi, mchezaji unahitaji kutengeneza muunganiko na mashabiki zako. Tumepewa vipaji tofauti, kwa hiyo kama unaweza kufanya jambo flani kwenye mpira tunasema umepewa kipaji hicho na Mungu, ni kipaji.

“Kwa hiyo ninachokifanya ni kutumia kipaji change nilichopewa na Mungu ili kukirudisha kwa mashabiki wanaokubali kile ninachokifanya ili wafurahie. Soka ni mabao na kushinda, kwa hiyo ukitumia kipaji chako kuipa ushindi timu yako linakuwa ni jambo jema.

“Baada ya kucheza hapa niliona video yangu ikitrend hapa Tanzania, sikujua ni kwa nini lakini baaadaye mashabiki wa Tanzania wakaanza kunifuata mtandaoni na kuniambia wanatamani nije kucheza hapa, mipango ya Mungu ndiyo imetimia.

“Ninawaomba mashabiki tuungane, tupambane tena msimu huu ili kubakisha mataji yetu ya ndani tuliyoshinda msimu uliopita na kufanya vizuri zaidi kimataifa. Siwezi kusubiri kuingia uwanjani na kuwapa furaha mnayoitarajia kutoka kwangu kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu, asanteni wananchi,”

SOMA NA HII  CHAMA ATUMIKA KUZUIA UBINGWA...SIMBA YAWAINGIZA CHAKA YANGA..KAZE ASHTUKIA ASUBUHI...