Home Habari za michezo ROBERTINHO AMPA MTIHANI HUU NGOMA

ROBERTINHO AMPA MTIHANI HUU NGOMA

Kocha Mkuu wa Simba SC, Olviera Robert ‘Robertinho’ amemwambia kiungo wake mshambuliaji Mkongamani, Fabrice Ngoma anataka kumuona akiifanyia makubwa klabu hiyo, katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ngoma ni kati ya wachezaji waliotambulishwa hivi karibuni na kuripoti kambini nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao ambao Simba SC inataka kuweka rekodi ya kufika hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mkongomani huyo tayari yupo kambini nchini Uturuki akiendelea kujiandaa chini kocha huyo ambaye amesimamia usajili wa mastaa wapya waliosajiliwa na timu hiyo.

Akizungumza mjini Ankara-Uturuki, Robertinho amesema kuwa anaamini kiwango cha kiungo huyo, hivyo anataka kumuona akitumia kiwango chake kutoa mchango katika timu ili wafikie malengo yao msimu ujao kimataifa.

Robertinho amesema kuwa, kiungo huyo ana CV kubwa ya kuzichezea klabu kubwa Afrika, hivyo ana uzoefu wa kucheza michuano mikubwa, anataka kumuona akitumia kipaji chake kuipa mafanikio Simba msimu ujao.

Amesema kuwa, kwa kushirikiana na wachezaji wenzake, anaamini ataifanyia mengi makubwa Simba SC huku akitoa nafasi ya kujiandaa zadi kwa kuongeza mazoezi ya fitinesi ili awe fiti zaidi ya hapo.

“Ngoma ni kati ya wachezaji ambao ninaowategemea kuelekea msimu ujao, nimempa kazi kubwa ya kuhakikisha anaipambania timu kutokana na uzoefu wake wa kucheza michuano mikubwa ya kimataifa.

“Kwani Ngoma amezipitia klabu kubwa nyingi ndani nje ya Afrika, hivyo ninamtegemea sana katika hawa wachezaji wapya ambao tumewasajili kwa ajili ya msimu ujao.

“Kwangu sina hofu naye kabisa, katika mchezo wa kirafiki wa tuliocheza Alhamisi, alicheza katika kiwango kikubwa, lakini hajaonyesha ubora wake ambao ninaufahamu,” amesema Robertinho.

SOMA NA HII  MAJANGA MASHABIKI SIMBA WATAKA ROBERTINHO AFUKUZWE, UNAAMBIWA SIMBA HAJASHINDA MECHI HATA MOJA KIMATAIFA