Home Habari za michezo KISA ONANA CHAMA AITABIRIA MAKUBWA SIMBA

KISA ONANA CHAMA AITABIRIA MAKUBWA SIMBA

CLATOUS CHAMA...MIMI KAMA MCHEZAJI SINA MANENO MENGI...NITAONYESHA VITENDO ZAIDI
CLATOUS CHOTA CHAMA MWAMBA WA LUSAKA

Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia na klabu ya Simba SC, Clatous Chama aibuka na kutamka kuwa ujio wa kiungo Willy Onana utaifanya timu hiyo, ifunge mabao mengi katika msimu ujao.

Onana ni kati ya viungo waliosajiliwa na Simba SC kwa ajili ya msimu ujao ambao wamepanga kurejesha makombe yote pamoja na kufika hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Akizungumza mjini Ankara-Uturuki, Chama amesema kuwa kwa siku chache ambazo amekaa kambini na Onana ameona ana kitu kikubwa ambacho atakifanya Simba SC msimu ujao 2023/24.

Chama amesema kiungo huyo anaonekana ana uchu wa kufunga mabao muda wote akiwa mazoezini na katika michezo ya kirafiki.

Ameongeza kuwa kikubwa kiungo huyo apewe ushirikiano mzuri kwa mashabiki ambao anaamini ndio watakaomfanya awe bora zaidi.

โ€œNipongeze usajili ambao umefanywa na viongozi wangu, kiukweli utatupa mafanikio makubwa msimu ujao.

โ€œNimefurahishwa na ubora wa kila mchezaji uwanjani, kati ya hao yupo Onana ambaye nimemuona anapenda sana kufunga kila anapopata mpira.

โ€œKikubwa mashabiki wampe muda wa yeye kuonyesha kipaji chake katika msimu katika kufanikisha malengo yetu,โ€ amesema Chama.

SOMA NA HII  KUELEKEA KESHO SIKU YA WANANCHI....PITSO MOSIMANE AIPA UJIKO YANGA...AAMUA KUPUMZIKA SOKA...