Home Habari za michezo USHINDANI WA MASTAA HAPO SIMBA SIO POA, MATOLA AMUIBIA SIRI MIQUISSONE

USHINDANI WA MASTAA HAPO SIMBA SIO POA, MATOLA AMUIBIA SIRI MIQUISSONE

Habari za Simba

SIMBA tayari imezindua Wiki ya Simba Day jijini Dar es Salaam, huku baadhi ya viongozi, wanachama pamoja na wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo wakijitolea kutoa damu kuchangia Mfuko wa Damu wa Taifa, huku mmoja ya wataalamu akimuonya nyota mpya Luis Miquissone.

Luis amerejeshwa kikosini katika dirisha la usajili lililopo wazi kwa sasa na tayari ameanza mambo katika kambi ya timu hiyo iliyopo Uturuki, lakini kocha wa zamani wa timu hiyo ambaye kwa sasa kahamishia makali yake kikosi cha vijana cha Msimbazi, Seleman Matola amemtahadhari mapema.

Kocha huyo wa vijana wa Simba, alisema licha ya Luis kuwa bado mchezaji nzuri, lakini anakibarua cha kufanya ili aweze kuwapa raha mashabiki wa klabu hiyo walio na matumaini makubwa naye.

Luis aliyeuzwa na Simba misimu miwili iliyopita kwa Al Ahly ya Misri na kuacha pengo kubwa katika kikosi hicho, amejereshwa baada ya kumaliza na mabosi wa klabu hiyo akipewa mkataba wa miaka mitatu na Matola aliyekuwa kocha msaidizi wa kikosi hicho alisema kurudi kwa mchezaji huyo kumerudisha furaha ya kila mwanachama wa Simba kwani alitolewa kishingo upande.

Hata hivyo, alinga nyota huyo wa kimataifa wa Msumbiji alisema Luis anakwenda kukutana na changamoto kuwa ya namba ukizingatia vitu vingi kama kocha na wachezaji ni wageni.

Aliendelea kusema mapokezi makubwa aliyopewa haimanishi kuwa ataishi kifalme kikosi ila anatakiwa kujua kuwa ana deni kubwa.

“Hakuna linalishindikana ila Luis anatakiwa asiishi kwa mazoea kwa Simba imebadilika na Kocha hataruhusu kumchezesha mtu wa kiwango cha kawaida.

“Simba imefanya usajili mkubwa ambao hauwezi kumpa amani mchezaji yoyote kujiona ananafasi ya kucheza wakati wote kwani kila mtu ni bora,” alisema Matola.

SOMA NA HII  KWA HAYA YANAYOENDELEA AZAM FC MNAPIGA HESABU VEMA LAKINI?