Home Habari za michezo BAADA YA ONYANGO KUONDOKA SIMBA, APATA SAPOTI KUTOKA RIVERS UNITED

BAADA YA ONYANGO KUONDOKA SIMBA, APATA SAPOTI KUTOKA RIVERS UNITED

Habari za Simba

Dar es Salaam. Siku chache baada ya kukamilisha usajili wa Joash Onyango kutoka Simba, Singida Fountain Gate iko mbioni kuinasa saini ya kiungo wa Rivers United ya Nigeria, Morice Chukwu.

Chukwu aliyeonyesha kiwango bora katika kikosi cha Rivers msimu uliopita ambao kiliishia hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, atatua nchini wiki hii ili kumalizana na Singida Fountain Gate itakayoshiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao.

Miongoni mwa wasimamizi wa mchezaji huyo alilifichulia gazeti hili kuwa Chukwu amekubali kujiunga na Singida Fountain Gate na kinachosubiriwa ni yeye kutua Tanzania na kusaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia timu hiyo.

“Timu nyingine hazikufikia makubaliano ndio maana Morice amechagua kuungana na Singida kwani ofa yao ndio imekuwa bora zaidi,” kilifichua chanzo hicho.

Mchezaji huyo alikiri mpango wake wa kuwasili Tanzania wiki hii lakini hakutaka kusema chochote kuhusu kwenda kuitumikia Singida Fountain Gate.

“Siwezi kusema chochote kwa sasa japokuwa ni kweli najiandaa kuja Tanzania siku ya Alhamisi ya wiki hii ila ni kwa mambo mengine na si hayo na kama ikitokea basi mtafahamu kila kitu ni swala la muda tu,” alisema Kiungo huyo.

Mkurugenzi wa Utawala,Muhibu Kanu, alisema kamati ya usajili inaendelea kutimiza wajibu wake na kama kutakuwa na lolote basi muda ukifika taarifa zote zitawekwa wazi.

Aidha alisema kuwa jukumu la Mchezaji mpya kusajili ni la kamati ya usajili ila kwani kila kamati inamajukumu yake ambayo yanatakiwa kuyafanya.

“Muda ukifika wa kamati ya usajili kumtangaza mchezaji mpya kila mtu atafahamu hivyo siwezi kutolea ufafanuzi kwani hicho sio kitengo changu ila tuendelee kusubiri tutajua tu,” alisema Muhibu Kanu.

Kama mpango wa kumsajili utakamilika, Chukwu atakuwa ni mchezaji wa saba kusajiliwa na timu hiyo hadi sasa akiungana na Nico Wadada, David Bryson, Joash Onyango, Habibu Kiyombo, Beno Kakolanya na Yahaya Mbegu.

Singida Fountain Gate ilimaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu msimu uliopita, jambo lililoifanya ikate tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao

Singida Fountain Gate ilimaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu msimu uliopita, jambo lililoifanya ikate tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE