Home Habari za michezo BARBARA AZIDI KUKINUKISHA SIMBA….AACHIA ‘DONGO’ LINGINE TENA …

BARBARA AZIDI KUKINUKISHA SIMBA….AACHIA ‘DONGO’ LINGINE TENA …

Habari za Simba

Siku maoja baada ya Rais wa heshima wa Simba SC, Mohammed Dewji kupost ujumbe ambao umezua sintofahamu kwa Mashabiki na wananchama wa Klabu ya Simba SC akidai kuchoka kutokana na kutokamilika kwa mchakato wa Transformation ndani ya Klabu ya Simba kwa miaka sita.

Juzi Julai 12, aliekuwa CEO wa Simba SC, Barbara Gonzalez ametweet ujumbe ambao umeacha maswali kwa walio wengi.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Barbara ameandika;

“Hauwezi kudhulumu haki za watu halafu ukataka amani na mafanikio.”

AKAJA NA HILI TENA

Mapema hii leo Julai 14, 2023, Barbara ameweka ujumbe mpya uliosomeka hivi:

“Ulevi wa madaraka haujawahi kuwa na mwisho mwema.”

Kama kawaida ujumbe huo umezua mjadala na watu kuhoji ni kitu gani kilichopo nyuma ya jumbe hizo zinazoonekana kama kuna watu anawalenga.

Kabla ya ujumbe huo, Barbara aliandika jumbe nyingine tata ambazo pia ziliibua mjadala wa kutosha.

“Usilipize ubaya kwa ubaya, lakini usiwe mnyonge kudai haki zako!”

“Hauwezi kudhulumu haki za watu halafu ukataka amani na mafanikio.”

SOMA NA HII  MASTAA SIMBA MGUU PANDE MGUU SAWA...WYDAD TUMBO JOTO...KOCHA AFUNGUKA HAYA