Home Habari za Simba MRITHI WA MANULA ATUA RASMI SIMBA, AHMED ATAMBA

MRITHI WA MANULA ATUA RASMI SIMBA, AHMED ATAMBA

Wakati Simba SC ikizindua jezi jana Ijumaa (Julai 21) usiku, Mlinda Lango Simon Omossola raia wa Cameron ametua Msimbazi kwa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo akitokea FC Saint Eloi Lupopo ya DR Congo.

Mashabiki wa Simba SC wakisubiri kwa hamu usajili wake, taarifa zinaelza kuwa kwa sasa klabu hiyo imebakiza kutambulisha majina mawili makubwa.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba SC kimesema kuwa Omossola na aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Luis Miquissone ndiyo majina pekee yaliyobaki kutambulishwa Msimbazi.

“Suala la kipa limekamilika ni nyakati tu zinazosubiriwa kwa ajili ya kumtangaza, mashabiki wapite kifua mbele usajili tulioufanya ni wa kufikia malengo tuliyoshindwa kuyafikia kwa misimu minne mfululizo kimataifa,” kimesema chanzo hicho.

Alipomtafutwa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally, amesema bado hawajafunga usajili, kuna wachezaji wawili wa kigeni muda wowote kuanzania sasa watatambulishwa baada ya kukamilisha taratibu zote.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA SIMBA ATOA MAAGIZO HAYA KWA MASTAA KABLA HAJATUA NCHINI