Home Habari za michezo RUNGU LA YANGA LATUA KWA BANGALA

RUNGU LA YANGA LATUA KWA BANGALA

Habari za Yanga SC

Rasmi Kiungo Mkabaji kutoka DR Congo, Yannick Bangala huenda asiwepo katika kikosi cha Young Africans cha msimu ujao hiyo ni mara baada ya jezi yake kukabidhiwa beki wa kulia mpya Muivory Coast, Attohoula Yao.

Bangala alikuwa akivaa jezi namba 4, katika misimu miwili mfululizo ambayo ameipa mataji sita mfululizo Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’, kila moja ametwaa mara mbili.

Yao amekabidhiwa jezi hiyo, mara baada ya kutambulishwa mwishoni mwa juma lililopita kama mchezaji mpya ambaye tayari yupo kambini akijiandaa na msimu mpya.

Awali ilielezwa kuwa Bangala yeye mwenyewe ameomba mkataba wake wa mwaka mmoja usitishwe ili aondoke akiwa pamoja na Shaaban Djuma.

Djuma yeye tayari anatajwa kujiunga na TP Mazembe ya DR Congo baada ya kufikia muafaka mzuri na uongozi wa Young Africans katika kuuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja.

Tayari beki huyo ameonekana kupitia katika kurasa za mitandao ya kijamii ya timu hiyo, akifanya mazoezi na jezi hiyo atakayoivaa msimu ujao.

SOMA NA HII  GAMONDI AFUNGUKA KILICHOOKOA JAHAZI DHIDI YA AZAM JANA