Home Habari za michezo SIMBA KIMEUMANA…KOCHA ATEMA CHECHE HATARI…YANGA WATAJWA

SIMBA KIMEUMANA…KOCHA ATEMA CHECHE HATARI…YANGA WATAJWA

SIMBA KIMEUMANA...KOCHA ATEMA CHECHE HATARI...YANGA WATAJWA\

KOCHA wa viungo wa Simba, raia wa Rwanda, Corneille Hategekimana ametoa onyo kali kwa wapinzani katika Ligi Kuu Bara wakiwemo Yanga  na kutakuwa na balaa zito watakapokutana kwa msimu mpya wa mashindano.

Amesema anashangazwa  na uwezo mkubwa wa wachezaji wa timu kuweza kuelewa  haraka mbinu za mazoezi  wanayowapa pamoja na Kocha Mkuu wa timu hiyo,  Roberto Oliviera (Robertinho).

Mtaalam huyo ametoa kauli hiyo kufuatia kuanza kazi rasmi ndani ya kikosi hicho kufuatia kambi ya walioweka nchini Uturuki   kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

Kocha huyo wa viungo alisema wamepata sehemu nzuri yenye ubora mkubwa wa kufanya maandalizi na tangu wamefika nchini humo ni siku nne ambazo wamefanya mazoezi  kwa wachezaji kuonekana kuelekea kwa haraka.

Alisema licha ya kutokamilika kwa wachezaji wote ndani ya kikosi anaimani kubwa mwisho ya Pre Season watakuwa vizuri zaidi , utimamu wa mwili, kiufundi na mbinu za uwanjani.

“Tangu tumefika hapa tulifanya maziezi ya viungo  Gym ,  tukaenda kwenye bwawa la kuongela ambalo kuna mazoezi yake ni muhimu na kumjenga mchezaji utimamu wa mwili na tumekuwa na programu ya uwanjani kwa kocha Robertinho kuanza kufanya majukumu ya mbinu na ufundi.

Tuko na timu nzuri sana wachezaji wameonyesha kuelewana vizuri kwa kile kinachotolewa kutoka kwetu wanajua nini wanatakiwa kufanya wanapokuwa  na mpira au hawana mpira jinsi ya kujilinda na mpinzani, huko mbele kutakuwa na kazi kubwa kwa wapinzani ,” alisema Hategekimana.

SOMA NA HII  SIMBA YAFANYA MAAJABU YAKE...KLABU BINGWA MIDOMO WAZI...RAJA CA HAWAAMINI MACHO YAO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here