Home Habari za michezo TRY AGAIN ATAMBA KUMSAJILI STRAIKA WA UHISAPANIA SIMBA HII SIO POA

TRY AGAIN ATAMBA KUMSAJILI STRAIKA WA UHISAPANIA SIMBA HII SIO POA

Mchezaji wa zamani wa CD Tenerife ya nchini Hispania, Shaban Chilunda
SIMBA wamefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa CD Tenerife ya nchini Hispania, Shaban Chilunda kwa mkataba wa miaka miaka miwili.

Chilunda ambaye ni zao la Azam, mwaka 2018 alitimkia Hispania katika klabu ya CD Tenerife kwa mkopo ambapo nayo ikamtoa tena kwa mkopo kwenda CD Izzara 2019 nayo ya nchini humo baadaye Tenerife walimrudisha Azam baada ya mkopo wake kumalizika.

Lakini msimu wa mwaka 2020, mshambuliaji huyo alijiunga na Klabu ya Moghreb Tetoun ya Morocco ambayo alidumu nayo kwa msimu mmoja kabla ya kurejea Azam katika mwaka 2022 ambayo iliachana naye kwenye dirisha dogo msimu huu.

Chanzo makini kutoka Simba kimeliambia Championi Jumatano kuwa, bado uongozi wa timu hiyo unaendelea na usajili wa wachezaji wazawa na Chilunda ameshamalizana na mabosi wa timu hiyo ambao muda wowote kutoka sasa watamtangaza kabla ya kuelekea katika kambi ya timu hiyo nchini Uturuki.

“Tunatambua ubora wa Chilunda tunaamini kwa wachezaji wazawa ataongeza nguvu ndani ya kikosi, tumeshakamilisha usajili wa nyota wawili wa ndani bado tuna nafasi moja, mpango wetu kuongeza nguvu eneo la beki wa kati na kunaongezeko la nyota wa kigeni.

“Uongozi kwa ujumla haujafurahishwa na kukosa mataji yote misimu miwili mfululizo, hivyo wameamua kushusha nondo za mastaa wa kutosha kwa ajili ya kulenga kufanya vyema katika mashindano yote ambayo timu itashiriki,” alisema mtoa taarifa.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema: “Wachezaji wapya wanaendelea kuwasili kambini, nawakumbusha tu hatujamaliza kusajili furaha zaidi itakuja hivi karibuni.”

Simba hadi sasa imesajili wachezaji watano, wanne kati yao ni wa kigeni ambao ni Essomba Onana, Aubin Kramo, Fabrice Ngoma na Che Malone Fondoh na mmoja mzawa, David Kameta.

SOMA NA HII  MAYELE AIKATAA YANGA HADHARANI MBELE YA MASHABIKI, ASEMA YEYE SIO SHABIKI WA YANGA, TIMU YAKE HII HAPA