Home Habari za michezo ALLY KAMWE ATAMBA, UONGOZI NAO WAWATAJA WAPINZANI

ALLY KAMWE ATAMBA, UONGOZI NAO WAWATAJA WAPINZANI

Habari za Yanga

UONGOZI wa Yanga, umebainisha kuwa, wapinzani watachagua mabao mangapi wafungwe watakapokutana kuanzia msimu wa 2023/24 kutokana na ubora walionao.

Ni Avic Town, Kigamboni, Dar, hapo ipo kambi ya Yanga wakiwa ni mabingwa watetezi wa Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports, mataji waliyobeba msimu wa 2022/23.

Akizungumza na chanzo chetu, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema: “Kwa namna ambavyo wachezaji wanajituma na wapo tayari kwa ajili ya msimu mpya, tutakuwa tunachagua wapinzani wetu tuwafunge mabao mangapi.

“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwenye kila wakati kwa kuwa wao sehemu ya mafanikio yetu unaona msimu wa 2022/23 tumefanya vizuri tunahitaji kuendelea kuwa bora zaidi.

“Msimu huu mpya tunakwenda kufanya kazi bora zaidi kwani kila mchezaji yupo tayari na benchi la ufundi pia linapenda kuona matokeo uwanjani tuzidi kuwa pamoja.”

SOMA NA HII  BAADA YA KIPIGO CHA JANA...MBRAZILI AJITETEA SIMBA...ADAI HAKUPATA MUDA WA KUANDAA TIMU...