Habari njema kwa mashabiki na wapenzi wa klabu ya SIMBA ni kunaswa kwa saini ya winga wa maana anayejua kazi na mbio mithiri zenye hatari kutoka Asec Mimosas, KRAMO AUBIN
Kramo (27) Msimu uliopita kwenye mechi za Kombe la Shirikisho, aliupiga mwingi na kufunga mabao manne
katika mechi tatu kati ya sita za hatua ya Makundi na timu hiyo kutolewa nusu fainali na USM Alger. Simba imefanikiwa kunasa saini yake baada ya kupambana kwelikweli na watani wao, Young Africans.