Home Yanga SC YANGA WASHINDWA KUTAMBA MALAWI WALAZIMBISHWA SULUHU

YANGA WASHINDWA KUTAMBA MALAWI WALAZIMBISHWA SULUHU

KLABU ya Yanga leo imelazimisha suluhu dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi katika mchezo maalumu wa kirafiki wa kimataifa kuadhamisha miaka 59 ya Malawi.

Mchezo huo uliohudhuriwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera umepigwa kwenye uwanja wa taifa wa Bingu uliopo mji mkuu wa Malawi, Lilongwe.

Timu zote mbili zilishambuliana kwa zamu lakini hakuna iliyoibuka na ushindi hadi mwisho wa mchezo huku Yanga ikichezea sehemu kubwa ya wachezaji vijana na wengine wapya.

SOMA NA HII  GAMONDI AFUNGUKA ISHU YA KONKONI KUANZIA BENCHI