Tetesi za Usajili Simba
Habari za michezo

ROBERTINHO AFUNGUKA KUHUSU SIMBA ALIYEITENGENEZA ISHU IKO HIVI KWENYE MATAJI

Staff Desk August 5, 2023 12:55 pm

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefurahi ubora wa kikosi tulichonacho kuelekea msimu mpya wa mashindano 2023/24 huku akiweka wazi malengo yetu ni kuchukua mataji ya ndani.

Kupitia dirisha hili kubwa la usajili Simba mpaka sasa imekamilisha usajili na kuwatangaza wachezaji tisa wapya wakiwemo mawinga, Luis Miquissone na Willy Onana ambao wanatajwa kuwa mastaa wanaotarajiwa kufanya makubwa.

Kikosi cha Simba juzi Jumatano alfajiri kiliwasili nchini kikitokea nchini Uturuki ambapo walikuwa na kambi ya siku tatu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya ‘Pre-season’.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kocha Mkuu wa Simba, Robert Olivieira alisema: “Baada ya kuwa na wiki tatu za maandalizi ya kabla ya msimu nchini Uturuki, naweza kusema nimeridhika na matokeo ya kambi tuliyoyapata kutokana na ubora mkubwa ulioonyeshwa na wachezaji.

“Ongezeko la wachezaji wapya limezidi kutupa machaguo mengi na kwa hili naupongeza uongozi wa klabu kwa kufanya usajili huu mkubwa. Simba ni timu kubwa na tuna malengo ya kuchukua ubingwa wa ndani na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.”

NGAO YA JAMII KUONYESHA MBIVU NA MBICHI, SIO SIMBA SIO YANGA…… ISHU IKO HIVI UONGOZI WA SIMBA WAFUNGUKA KUHUSU SAMIA KUWA MGENI RASMI ISHU IKO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “ROBERTINHO AFUNGUKA KUHUSU SIMBA ALIYEITENGENEZA ISHU IKO HIVI KWENYE MATAJI”

  1. Lutufyo sambo says:

    Uhakika

Leave a Reply