Habari za Simba SC
Habari za michezo

BAADA YA KUWASASAMBUA WAZAMBIA JANA…MBRAZILI SIMBA KATIKISA KICHWA KISHA AKASEMA HILI…

admin August 7, 2023 12:16 pm

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Power Dynamos kwenye kilele cha Simba Day.

Robertinho amesema kikosi chake  kinazidi kuimarika siku hadi siku na wachezaji wanazidi kuzoeana kitu ambacho kinampa wigo mpana wa uchaguzi wa timu.

Robertinho ameongeza kuwa wachezaji wapya waliosajiliwa wameonyesha uwezo mkubwa na wanazidi kuzoea mazingira ya timu pamoja na wenzao.

“Nimefurahishwa na kiwango cha timu, tumecheza vizuri na timu inazidi kuimarika. Tuna kikosi kizuri.

“Hata wachezaji wapya tuliowasajili wameonyesha uwezo mkubwa, na wanazidi kuzoea mazingira mapya pamoja na wenzao,” amesema Robertinho.

Robertinho amewashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la Simba Day na kulifanya kupendeza zaidi.

WAKATI SIMBA WAKIHAHA NA MBADALA WA MANULA….GAMONDI NA YANGA YAKE NI KICHEKO TU… BAADA YA KURUDI RASMI NA KUKIWASHA JANA…MIQUISSONE APEWA ZA USO KWA UNENE WAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply