Habari za michezo
BAADA YA KURUDI RASMI NA KUKIWASHA JANA…MIQUISSONE APEWA ZA USO KWA UNENE WAKE…
admin
August 7, 2023
12:21 pm
Wakati kwa mara ya Kwanza wachezaji wa Simba wakonekana hadharani jana Agosti 6 katika kilele cha Tamasha la “Simba Day” katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Power Dynamos ya Zambia
Wapo nyota kadhaa wageni ambao wamesajiliwa dirisha hili wameonekana kuanza na moto mkubwa kama Straika Willy Onana na Kiungo Fabrice Ngoma ambao walianza kwa kutupia magoli katika mchezo wa jana.
Nyota alieteka hisia za wengi katika usajili wake ni Jose Luis Miquissone ambae nae alipata nafasi ya kucheza mchezo wa jana kwa dakika chache.
Sasa Mchambuzi wa Michezo kutoka TV3 Alex Ngereza ambae hapo awali alipingana na usajili wa mchezaji huyo amezungumza kuhusu kiwango kilichooneshwa na Miquissone jana;
“Kiwango cha Miqusson kimeshuka sana sidhani kama anaweza kurudi kwenye ubora wake kwasababu hata hivyo amekuwa mnene sana tofauti na alivyokuwa kipindi cha nyuma”
Je una neno lipi la kumwambia Mchambuzi Alex Ngereza? Unakubaliana na maoni yake?
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.