Home Habari za michezo ROBERTINHO AFUNGUKA JINSI SIMBA WALIVYOBADILISHA MBINU KATIKA MCHEZO WA JANA, CHANZO CHA...

ROBERTINHO AFUNGUKA JINSI SIMBA WALIVYOBADILISHA MBINU KATIKA MCHEZO WA JANA, CHANZO CHA SUB ZOTE ZILE NI HII

Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’ raia wa Brazil amesema kuwa aliwabadilishia mbinu wapinzani wake Power Dynamos ya Zambia kwenye mchezo wa kirafiki wa Simba Day jana Agosti 6, 2023.

Robertinho amesema hayo jana mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambapo Simba wakiwa katika Dimba la nyumbani, Kwa Mkapa waliibuka na ushindi wa bao 2-0.

“Wachezaji wangu wamecheza vizuri, malengo yangu ni kuwa Bingwa msimu huu. Kwa sasa tuna wachezaji wa daraja la juu kwenye kikosi chetu. Nimetumia mpango tofauti kpindi cha kwanza kisha nikabadilisha mpango kipindi cha pili.

“Kipindi cha kwanza nimecheza kwa kushambulia zaidi kila wakati, kipindi cha pili nikacheza kwa kukaba na kushambulia mara chache. Hivi ndivyo navyotaka timu yangu iwe, tuendane na mifumo tofauti kulingana na mpinzani tunayekutana naye ili tufikie malengo yetu,” amesema Kocha Robertinho.

Katika mchezo huo, Robertinho hakuanza na mshambuliaji kwenye kikosi chake;

Ally Salim

Shomary Kapombe

Mohamed Hussein

Henock Inonga

Che Malone

Sadio Kanoute

Leandrew Onana

Clatous Chama

Kibu Denis

Saido Ntibazonkiza

Mzamiru Yasin.

Baadaye aliwaingiza Jean Baleke, Fabrice Ngoma, John Bocco, Luis Miquissone kwa nyakati tofauti.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA MASHABIKI KUSHINDWA KUANGALIA MECHI RWANDA, UONGOZI WA YANGA WASEMA HAYA