Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga SC, Fiston Mayele, amefunguka kuwa, wakati Feisa Salum alipotaka kuondoka Yanga, alimshauri asiondoke.
Hilo limejidhirisha kupitia documentary ya Yanga waliyoizindua hapoa jana Agosti 7, 2023.
“Mimi Feisal ni rafiki yangu, najua mambo yake anajua mambo yangu, nakumbuka maneno ya yeye kuondoka Yanga alianza kuniambia wakati tunaenda kucheza mechi ya marudiano na Club Africain.
“Lakini mimi nilimwambia usiondoke wakati huu (ule), subiri msimu uishe ndio uondoke, nilimwambia wewe umecheza hii Timu kwa muda mrefu subiri huu msimu uishe ndio uondoke,” Fiston Mayele akizungumza kwenye Documentary ya Yanga Sc.
SOMA NA HII KUELEKEA MECHI YA KESHO SIMBA vs AL AHLY...JEMEDARI SAID ATUPA KOMBORA HILI KWA YANGA...