Habari za michezo
CHAMA, MOLOKO KUIKOSA NGAO YA JAMII ISHU IKO HIVI
Staff Desk
August 9, 2023
11:27 am
Klabu ya Simba SC itamkosa kiungo wake, Clatous Chama kwenye michezo ya ngao ya jamii dhidi ya Singida Fountain Gate kesho Alhamisi, Agosti 10, 20230 katika Dimba la Mkwakwani.
Chama anatumikia adhabu ya kutocheza mechi (3) alizofungiwa na bodi ya ligi msimu uliopita kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu.
Pia, Klabu ya Yanga itamkosa winga wao, Jesus Moloko kwenye mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Azam FC leo Jumatano, Agosti 9, 2023 hapo hapo katika Dimba la Mkwakwani.
Moloko pia anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyooneshwa kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City msimu uliopita.
Comments:
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.