Home Habari za michezo GAMONDI ATAMBA, YANGA BADO HAWAJAANZA KUTUMIA MIFUMO YAKE

GAMONDI ATAMBA, YANGA BADO HAWAJAANZA KUTUMIA MIFUMO YAKE

Habari za Yanga SC

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi licha ya timu yake kupata matokeo dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii, amesema kuwa timu hiyo inahitaji muda kidogo kucheza katika mifumo yake.

Yanga katika mchezo huo walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Aziz Ki na Clement Mzize kwenye kipindi cha pili pale Dimba la Mkwakwani na sasa wametinga fainali ambayo watacheza na mshindi kati ya Simba dhidi ya Singida FG ambao walicheza.

Kocha Gamondi huu ni msimu wake wa kwanza ndani ya Yanga akiwa anachukuwa nafasi ya kocha Nassredine Nabi, ambaye kwa sasa amejiunga na klabu ya Far Rabat ya nchini Morroco.

Akizungumza na Championi Ijumaa, hapa mkoani Tanga, Kocha Gamondi alisema kuwa amefurahishwa na matokeo ambayo wameyapata katika mchezo wao huo wa kwanza muhimu, wanachoangalia kwa sasa ni kuona wanapata matokeo mazuri pia katika mchezo ujao.

Aliongeza kuhusu uchezaji wa timu bado kidogo mbinu zake hazijawaingia vizuri wachezaji jambo ambalo linahitaji muda kuipata Yanga anayoitaka.

“Jambo la kwanza ambalo nimefurahiswa nalo ni kuhusiana na matokeo ambayo tumeyapata hakika ni jambo jema kwetu wote wachezaji na mashabiki, ni matokeo ambayo tuliyahitaji.

“Kikubwa ni kwenda kupata matokeo pia katika mchezo ambao unafuata, kuhusu uchezaji wa timu bado tunahitaji muda ili wachezaji kucheza katika mbinu na mifumo yangu, naamini kuna kitu kipo na kimeanza kufanyiwa kazi ila inahitaji muda ili kuwa katika asilimia zote kuifikia Yanga ambao naihitaji,” alisema kocha huyo.

SOMA NA HII  AL MAREIKH TUMBO JOTO,GAMONDI AMVURUGA KOCHA