Timu zote zimetoka kucheza mechi za Nusu Fainali na kufanikiwa kufuzu kucheza Fainali, kuuendea mchezo wa Fainali ya watani wa Kariakoo itakuwa tofauti na ambavyo waliingia kwenye mechi za Nusu Fainali.
Mechi ya watani huamsha ari kwa wachezaji ambayo wakati mwingine hupelekea kuziba baadhi ya madhaifu/mapungufu ya timu kutokana na hamasa kuelekea mechi hiyo.
Ukimsikiliza Kocha wa Simba, Robertinho anasema timu yake itacheza kwenye eneo la mpinzani lakini kwenye mechi ya Singida Fountain Gate FC kitu hicho hakikuonekana.
Simba iliruhusu mipira mingi kupita katika eneo lao la katikati na kwenda hadi kwenye eneo lao la mwisho la kujilinda, kwa walinzi wa kati au kwa golikipa.
Yanga kwenye mechi yao dhidi ya Azam FC walifanikiwa kuwafinya Azam kuanzia kwenye eneo lao la kwanza na kufanikiwa kupata nafasi nyingi kupitia presha ambayo walikuwa wanawatengenezea Azam.
Kama Yanga wataweza kutia hiyo presha kwa Simba na kuwalazimisha kupoteza mipira kwenye eneo lao la kwanza, inaweza kuwa faida kwa Yanga.
Wachezaji wa Yanga wameonekana kukimbia zaidi wakati timu yao haina mpira kwenye mechi zao za hivi karibuni tangu timu iwe chini ya Gamondi.
Aaaaaaah good san lig kuanz