Habari za Yanga
Habari za michezo

KWA RATIBA HII SASA YANGA WASHINDWE WENYEWE

Staff Desk August 13, 2023 3:28 pm

YANGA ishindwe yenyewe tu kwa namna neema ilivyoiangukia mapema kabla ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na michuano ya CAF haijaanza kutokana na ratiba ilivyowakalia utamu.

Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuanza Agosti 15 na Yanga imepangwa kuanzia nyumbani katika mechi tatu mfululizo, kisha hata kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ikipata ulaini kwa kutakiwa kucheza zote jijini Dar es Salaam.

Yanga itaanza Ligi Kuu dhidi KMC, kisha kuialika JKT Tanzania na Namungo zote hizo zitapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, wakati huo huo za CAF Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Asas FC ya Djibouti zote zitapigwa hapohapo.

Sababu ya Djibouti kuomba mechi ya nyumbani na ugenini kucheza Tanzania zinatajwa ni viwanja vyao kutokidhi kanuni za FIFA, hivyo ni faida kwa Yanga kujipanga zaidi kutumia uwanja wa nyumbani.

Yanga mara baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii watarudi kujiweka sawa na mchezo wao wa hatua ya kwanza unaotarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 18-20 dhidi ya Asas FC ya Djibouti.

Lakini taarifa mbaya kwa Yanga ni kwamba Simba itamalizia mechi zake zote tatu za ligi nyumbani katika mbio za ubingwa.

ISHU YA SINGIDA KUSHIRIKIANA NA YANGA KUIMALIZA SIMBA IKO HIVI KUHUSU SIMBA KUTUMIA BILIONI 3 KWA KIPA MPYA….?, UKWELI WOTE HUU HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply