Habari za Simba
MWENYEKITI WA SIMBA SC AFARIKI DUNIA
Staff Desk
August 15, 2023
10:46 am
SIMBA SC imetangaza kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Ayubu Saleh Chamshama aliyefariki Agosti 11, 2023 akiwa hospitali nchini India.
Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Soud Chamshama msiba utakuwa nyumbani kwake Chang’ombe Maduka Mawili.
Aidha, mazishi yatafanyika Leo kijiji cha Kilole Lushoto mkoani Tanga.
Uongozi wa Simba umetoa pole kwa ndugu, jamii na marafiki walioguswa na msiba.

Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.