Habari za michezo

MSEMAJI WA YANGA AWAAMBIA HAYA AL MARREIKH KIMATAIFA

Staff Desk August 26, 2023 12:06 pm

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe ameitaka Klabu ya Al-Merreikh ya Sudan kusema mapema kuwa mchezo wao wa Kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika watachezea nchi gani.

Kauli hii ya Kamwe inakuja baada ya Merreikh kufanikiwa kufuzu hatua ya pili ya mtoano baada ya kuiondoa Otôho d’Oyo FC ya Congo Brazzaville jana Ijumaa huku Yanga ikiwa na kibarua leo Jumamosi, Agosti 26, 2023 mbele ya ASAS FC ya nchini Djibouti.

“Tuna hasira na Wasudan, mwaka jana tulitolewa Klabu Bingwa na Al Hilal, kwa hiyo mwaka huu tutalipa kisasi. Huyu Al-Merreikh amejileta mwenyewe, acha tumalizane na ASAS kwanza kisha tumfuate kwake.

“Uzuri wa Yanga haisubiri kushinda nyumbani, tutaanzia kwake kisha tutamalizan nae hapa kwetu. Sasa atume location mapema atachezea wapi kwa sababu hachezei nchini kwao.

“Yanga ya sasa hivi sio timu ya kupaki basi, huko huko wanakochezea tutawapelekea moto,” amesema Kamwe.

Ikumbukwe kuwa, Yanga leo itacheza na ASAS katika Dimba la Azam Complex Chamazi Dar huku Wananchi wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wa kwanza ulipigwa uwanjani hapo Jumapili iliyopita hapo hapo Chamazi kwa bao 2-0.

SIRI TATU ZA AZIZI KI,….. MBRAZILI ASHTUKIA JAMBO SIMBA AZAM COMPLEX KUANZIA SASA IITWE YANGA COMPLEX ALLY KAMWE AFUNGUA HAYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply