JKT TANZANIA WAENDELEZA UONEVU
Habari za michezo

JKT SIO KINYONGE MBELE YA YANGA JAPO USHINDANI NI MKALI

Staff Desk August 27, 2023 5:10 pm

Kikosi cha JKT Tanzania kinaendelea na mazoezi kujiwinda na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga utakaopigwa keshokutwa, huku kocha mkuu wa timu hiyo, Malale Hamsini akiweka bayana ameandaa programu maalumu ya kuwafuatilia wapinzani wake.

JKT imerejea Ligi Kuu msimu huu kutoka Championship sambamba na Mashujaa na Kitayosce, na ilianza kwa ushindi wa bao 1-0 ikiwa ugenini Lindi dhidi ya Namungo na keshokutwa Jumanne itakutana na Yanga kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Malale alisema baada ya kuanza vyema ligi msimu huu anataka kuwa na mwendelezo kwa wachezaji, licha ya kukiri anakwenda kukutana na ushindani mkali.

WAKATI BODI YA LIGI WAKIIKATALIA SIMBA KUCHEZA NA COSTAL…MBRAZILI KAAMUA KUJA NA GIA HII… ROBERTINHO APIGA HESABU SIKU HIZI HAPA 16

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply