Home Habari za michezo WAPINZANI WAIPIGIA SALUTI YANGA…WAFUNGUKA HAYA

WAPINZANI WAIPIGIA SALUTI YANGA…WAFUNGUKA HAYA

Klabu ya ASAS ya nchini Djibouti imeukubali mziki wa Yanga Sc baada ya kupokea kichapo cha bao 5-1 katika mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa jana Agosti 26 2023 katika Dimba la Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, mchezaji wa ASAS, Gilbert Kaze raia wa Burundi ambaye amewahi kuichezea Simba Sc msimu wa 2013, amesema Yanga ni timu kubwa hivyo walistahili ushindi.

“Mchezo ulikuwa mzuri, lakini ukweli ni kwamba Yanga ni timu kubwa Afrika, ina wachezaji wengi wenye wazuri na uwezo mkubwa, asilimia kubwa ya wachezaji wake wamekaa pamoja kwa muda mrefu, mechi mbili wamecheza mpira mkubwa na wametuzidi.

Mchezaji wa ASAS FC, Gilbert Kaze. “Timu yetu sisi wengi wetu ni vijana, tumejitahidi kadiri ya uwezo wetu lakini Yanga walituzidi, tumecheza vizuri ila Yanga walikuwa bora zaidi yetu ndio maana wameshinda, kifupi niseme Yanga ni timu nzuri,” amesema Kaze.

Baada ya ushindi wa jumla wa bao 7-1, Yanga sasa itakutana na Al-Merreikh ya Sudan katika raundi ya pili ya mtoano ya michuano hiyo ambapo Wananchi wataanzia ugenini nchini Rwanda kisha kumaliza shughuli yao hapa Tanzania.

Je, Yanga wataweza kuvunja mwiko wa kutoingia makundi kwa miaka 25 sasa?

SOMA NA HII  GAMONDI AWAPOTEZEA SIMBA, ASEMA HAYA KUHUSU YANGA KUKUTANA NA SIMBA