Home Habari za michezo BEKI LA SIMBA LAPAGAWA NA KINA PACOME, MAXI AFUNGUKA HAYA

BEKI LA SIMBA LAPAGAWA NA KINA PACOME, MAXI AFUNGUKA HAYA

Habari za Yanga SC

Kikosi cha ASAS kimetimka nchini kurejea Djibouti wakiwa wameng’oka michuano ya CAF baada ya Yanga kuifumua jumla ya mabao 7-1, lakini beki mmoja wa zamani wa Simba ameacha salamu alichokiona Chamazi ni Vijana wa Jangwani wana watu na wapinzani watapata tabu sana.

Beki huyo anayekipiga timu hiyo kwa sasa, Gilbart Kaze aliyewahi kuifunga Yanga akiwa na Simba, Oktoba 2013 aliliambia Mwanaspoti kama kuna timu inawadharau mabingwa hao Watanzania watakutana na kitu kizito kwani jamaa wana timu bora iliyokamilika kila idara.

Kaze alisema licha ya kucheza mechi moja tu kati ya mbili dhidi ya Yanga katika mechi za raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini amekikubali kikosi hicho akisema kinaundwa na wachezaji wenye viwango vikubwa ambao karibu wote hawajapishana sana kwa ubora.

Raia huyo wa Burundi alisema licha ya Yanga kuchezesha vikosi viwili tofauti kwenye mechi hizo mbili walizovcheza nao kisha kupoteza kwa jumla ya mabao 7-1 ubora waliouonyesha kwao hana wasiwasi watapata mafanikio makubwa msimu huu kwa Tanzania na hata nje.

“Sisi Asas tunayachukua matokeo haya kama njia ya kujifunza lakini kwa timu zingine niwaambie Yanga wana timu bora, kikosi chao kina wachezaji bora sana wenye ufundi mkubwa,” alisema Kaze ambaye aliifunga Yanga bao la tatu kwenye sare ya mabao 3-3 baada ya Simba kuwa nyuma dakika 45.

“Angalia kwenye mechi zetu hizi mbili wametumia vikosi viwili tofauti hii mechi ya jana (juzi) walitumia wachezaji wanne tu waliocheza mchezo wa awali, ila angalia bado unaona ubora wa timu haujabadilika kabisa,” alisema Kaze na kuongeza;

“Wana wachezaji mafundi sana hasa eneo la katikati ya uwanja hata kule kwenye mabeki wao ni wachezaji waliokomaa vizuri, nakubaliana na timu yetu sisi haikuwa ngumu kwao lakini kitu chenye ubora kinaonekana mapema.

Akizungumzia ubora wa wachezaji mmoja mmoja Kaze alisema amekoshwa na viwango vya wachezaji kama Stephane Aziz KI, Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli na mabeki Yao Kouassi na Dickson Job.

“Hao ni wachezaji wazuri sana muangalie Aziz KI kila akigusa mpira kama hujatulia kwa kumsoma atakupa shida, yule Zouzoua (Pacome) naye mpira ukiwa miguuni kwake ana akili sana na ufundi kwa mabeki naona yule Yao (Kouassi) ni beki bora sana ana kila kitu hata yule Job (Dickson) alicheza mechi ya kwanza naye ana akili sana.”

Yanga sasa itacheza na El Merrikh ya Sudan katika mechi za raundi ya kwanza ikianzia Morocco ambapo wasudan wamechagua kuicheza mechi ya nyumbani kati ya Septemba 15-17 kisha kurudiani wiki moja baadaye jijini Dar es Salaana na mshindi kutinga makundi. Yanga mara ya mwishi kucheza makundi ya Ligi ya Mabingwa ilikuwa mwaka 1998 ikiwa na maana ni miaka 25 iliyopita.

SOMA NA HII  AZAM COMPLEX KUANZIA SASA IITWE YANGA COMPLEX ALLY KAMWE AFUNGUA HAYA