Home Habari za michezo EDO AWAITA MASHABIKI WA SOKA, AFUNGUKA MAZITO KUHUSU YAO WA YANGA

EDO AWAITA MASHABIKI WA SOKA, AFUNGUKA MAZITO KUHUSU YAO WA YANGA

Habari za Yanga SC

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Edo Kumwembe amemsifia beki mpya wa kulia wa Yanga, Kouassi Attoula Yao kutokana na kiwango chake kuwa bora na kuwavutia mashabiki na wapenda soka nchini.

Edo amesema hayo jana Jumapili, Agosti 20, 2023 kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa hatiua ya awali wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Yanga na ASAS FC ya Djibouti ambapo Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-0.

Yao amesajiliwa msimu huu na Yanga akitokea Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast lakini tangu atue Jangwani ameonyesha kiwango bora jambo ambalo limekosha Wananchi.

“Gongowazi mwambieni huyu beki wenu sijui anaitwa Yao Yao apunguze kuwa serious sana, sisi mpira wetu tunataniana tu. Mbona yupo serious sana kama anadai madeni ya vikoba? Bonge la defender aisee! Top class,” amesema Edo Kumwembe.

SOMA NA HII  YANGA FUNGA MWAKA INAFANYIKA HIVI