Home Habari za michezo GAMONDI APATA WASIWASI, PACOME, MAXI WAZUO HOFU, ISHU IKO HIVI

GAMONDI APATA WASIWASI, PACOME, MAXI WAZUO HOFU, ISHU IKO HIVI

Habari za Yanga

MIGUEL Gamondi ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga, ameibuka na kusema kuwa, mapumziko ya muda mrefu huenda yakamfanya kuanza upya kukisuka na kuwaongezea fitinesi ambayo wanayo kwa sasa wachezaji wake.

Yanga imeonekana kuimarika katika kila mchezo iliocheza, kwa wachezaji wake kucheza katika kiwango bora sambamba na kupata ushindi mnono.

Timu hiyo inayoundwa na mastaa wapya akiwemo Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua, Kouassi Yao na Skudu Makudubela, wameonekana kucheza katika kiwango kikubwa tangu wajiunge na timu hiyo.

Hofu ya Gamondi ni kusimama kwa Ligi Kuu Bara kwa takribani wiki mbili kuanzia leo Alhamisi mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Singida Fountain Gate dhidi ya Kitayosce FC, kupisha michezo ya kufuzu AFCON.

Akizungumza na Spoti Xtra, Gamondi alisema, michezo minne ya kimashindano waliyocheza, imewaongezea mastaa wake ufiti, huku akilia na mapumziko yaliyopo mbele yao yatashusha morali kwa wachezaji.

Gamondi aliitaja michezo miwili dhidi ya ASAS FC na ule wa KMC umemsaidia kuimarisha kikosi chake kabla ya kukutana na JKT Tanzania juzi Jumanne.

“Kikosi changu kipo imara, sina wasiwasi na michezo inayofuatia ya ligi na kimataifa, nimewaandaa wachezaji wangu kwa ajili ya kushindana na wamekuwa wakifanya kile ninachowaelekeza.

“Kikubwa tunahitaji ushindi katika kila mchezo utakaokuwa mbele yetu, ninataka kuona timu ikipata ushindi mkubwa na soka safi la kuvutia ili mashabiki wapate burudani.

“Lakini nimeingia hofu na haya mapumziko marefu, kwani yanaweza kupelekea kuanza upya, kutokana na sifa za wachezaji kutokuwa pamoja ndani ya muda, kwani wengi wao ni wapya.

“Nahofia wachezaji kupunguza fitinesi iliyopo hivi sasa, kama unavyofahamu wachezaji ni kama watoto wasipoelekezwa nini wafanye wanajiachia na kufanya mambo ambayo kisoka ni lazima waanze moja,” alisema Gamondi.

SOMA NA HII  HII SASA KALI SIMBA YACHUKUA POINTI TATU NJE YA UWANJA