Home Habari za michezo KUELEKEA MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA….CAF WASHUSHA WARAKA HUU KWA SIMBA NA...

KUELEKEA MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA….CAF WASHUSHA WARAKA HUU KWA SIMBA NA YANGA…

Habari za michezo

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limezipongeza klabu za Tanzania zinazocheza mashindano ya kimataifa kwa kukidhi vigezo vya Leseni za Klabu (Club Licensing), hivyo kupata leseni za kucheza mashindano hayo.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezipatia leseni klabu za Yanga na Simba zinazocheza Ligi ya Mabingwa, na Azam FC na Singida Big Stars zinazocheza Kombe la Shirikisho baada ya kukidhi vigezo.

Kutokana na Kamati ya Leseni za Klabu ya TFF kuzipatia leseni klabu hizo, CAF nayo imehuisha leseni hizo ili timu za klabu hizo zicheze mashindano yake kwa msimu wa 2023/2024.

Hata hivyo, CAF imezikumbusha klabu hizo kuwa kwa mujibu wa Kanuni yake ya Leseni za Klabu ya 2022, zinatakiwa kutekeleza vigezo na masharti yote ya kanuni hiyo kwa msimu mzima, na ikitokea zimekiuka, leseni hizo zitafutwa.

SOMA NA HII  BASI LA SIMBA SC LAWEKWA SOKONI