Home Habari za michezo MBRAZILI SIMBA APITISHA ‘TIKI YA KIJANI’ KWA LUIS MIQUISSONE NA PHIRI…ISHU NZIMA...

MBRAZILI SIMBA APITISHA ‘TIKI YA KIJANI’ KWA LUIS MIQUISSONE NA PHIRI…ISHU NZIMA IKO HIVI..

Habari za Simba

Nyota wa Simba, Luis Miquissone na Moses Phiri huenda wakaanza kuonekana mara kwa mara kikosini kutokana na kiwango walichokionyesha katika mchezo wa juzi dhidi Dodoma Jiji.

Simba ilipata ushindi wa pili mfululizo katika Ligi Kuu kwa kuifunga Dodoma Jiji mabao 2-0, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ingawa kiwango kilikuwa tatizo kwa michezo mitatu iliyopita ya mashindano yote.

Baada ya kupita miezi nane, Phiri alifunga bao kwenye Ligi Kuu tangu Desemba mwaka jana na baada ya hapo alipitia misuko suko ikiwemo majeraha na kushindwa kupata nafasi ya ndani ya kikosi cha kocha Oliveira Roberto ‘Robertinho’.

Miquissone aliyewahi kuwika na Simba msimu wa 2020/21, akifunga jumla ya mabao tisa na asisti 15, kwenye mashindano yote kabla ya kuuzwa kwa Al Ahly ya Misri, ambako mambo hayakumwendea vizuri na kuamua kurejea Msimbazi msimu huu.

Ubora walioonyesha wawili hao juzi ulimkuna Robertinho, ambaye alisema ni matokeo ya maandalizi wanayofanya kwenye viwanja vya mazoezi na kuweka wazi katika mechi zijazo wawili hao watapewa muda zaidi wa kucheza.

“Tangu msimu unaanza nilisema, kikosi chetu kina wachezaji wa aina mbili, wapo ambao wapo tayari kwa mechi, lakini wengine bado hawajawa kamili kwa asilimia 100.

“Miongoni mwa hao ambao walikuwa wakihitaji muda zaidi ili wacheze vizuri ni Phiri na Luis, lakini kila tunavyofanya mazoezi wanazidi kuimarika kama ulivyowaona na sasa naweza kumtumia yeyote kati yao kwa dakika zote 90.

“Nimefurahishwa na kiwango chao cha leo (juzi), sasa ni wakati wao kuonyesha zaidi kile walichonacho, nitawapa muda kwa kadri watakavyonishawishi, najua ni wachezaji wenye uwezo mkubwa na wataisaidi Simba msimu huu kufikia malengo,” alisema Robertinho.

Aidha, kocha huyo raia wa Brazil alisema hana shida na Phiri kama baadhi ya watu wanavyosema, lakini kilichofanya mara nyingi akose muda wa kucheza kikosini ni ushindani wa namba kuwa mkubwa.

Kukipiga Ijumaa
Baada ya ushindi dhidi ya Dodoma Jiji, Simba inatajwa kuomba mchezo wake dhidi ya Coastal Union, ambao awali haikuwa umepangiwa tarehe, uchezwe Ijumaa na tayari ombi hilo limekubaliwa na Bodi ya Ligi (TPLB).

Simba ingekaa bila mchezo hadi Oktoba 3, ambayo ingecheza na Tanzania Prisons ugenini, jambo ambalo benchi la ufundi limeona ni mbali na kuomba kucheza mchezo na Coastal, ambao haikupangiwa tarehe kutokana na muingiliano wa mechi za kimataifa.

Baada ya Bodi kukubali ombi hilo la Simba, kikosi hicho kiliahirisha mapumziko ya siku moja ambayo wachezaji walikuwa wamepewa na jana walirejea mazoezini kujiandaa na mechi hiyo ya tatu kwenye ligi msimu huu, ambayo huenda Phiri na Miquissone wakapata muda wa kuanza.

SOMA NA HII  KAKOLANYA AGOMEA WITO WA KAMATI YA NIDHAMU SINGIDA BS...HAMNITTENDEI HAKI ISHU NZIMA HII HAPA