Home Habari za michezo SIMBA WAITAMANI COASTAL UNION….. ISHU YAFIKA BODI YA LIGI

SIMBA WAITAMANI COASTAL UNION….. ISHU YAFIKA BODI YA LIGI

Habari za Simba SC

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wamekiri kuwaandikia bodi ya Ligi barua ya kuomba wacheze raundi ya tatu mechi dhidi ya Coastal Union.

Akizungumzia suala hilo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema Bodi ya Ligi waliuweka ‘pending’ mchezo huo wakidhani Simba wataanzia hatua ya awali katika michezo ya Kimataifa lakini bahati nzuri hawakuanzia.

“Ilikuwa tusicheza raundi ya tatu kutokana na kudhani tutaanzia hatua ya awali Klabu Bingwa lakini bahati nzuri hatukuanzia hatua hiyo.

“Ukiangalia ratiba tuna mchezo mwingine tarehe tatu mwezi wa kumi. Tumeomba watupe mechi na Coastal Union ili kuepuka viporo huko baadaye. Bodi nadhani wataangalia na wenzetu nafasi yao ili kama wana nafasi nzuri basi tutacheza watakapoturuhusu, sisi tupo tayari na ndio maana tukaomba tupangiwe wiki hii,” alisema Ahmed.

SOMA NA HII  YANGA YAMALIZANA NA MASHINE TANO... WAWILI WAFICHWA...SAKHO AWAGAWA MABOSI SIMBA..