Home Habari za michezo ROBERTINHO AFUNGUKA KUHUSU SOKA ANALOLITAKA SIMBA

ROBERTINHO AFUNGUKA KUHUSU SOKA ANALOLITAKA SIMBA

Habari za Simba leo

Kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’, amesema anataka kuona wachezaji wake wakicheza mpira mzuri na tayari ameanza anaona muelekeo wa kikosi chake kucheza soka ambalo analitaka kuliona msimu huu.

Simba juzi ilifanikiwa kukusanya alama tatu zingine kwa kuibuka na ushuindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma jiji FC, ambao umepigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Robertinho alisema wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu wanapewa nafasi na wanaonyesha uwezo mkubwa ambapo wanaingia taratibu kikosini.

Alisema nyota wapya na wale waliokuwepo awali wameweza kutengeneza muunganiko mzuri na kupata muelekeo wa timu yake kucheza soka ambalo analihitaji la ‘Samba Loketo’.

“Nahitaji kuona mpira mzuri, mpira sio ugomvi ni kipaji na Sanaa, napenda zaidi kushambulia zaidi na kucheza mpira mzuri, matarajio yangu muda mfupi naweza kupata muelekeo wa kile ninachokitaka katika kikosi changu.

“Nimefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wangu hasa wale tuliowasajili msimu huu wanaonyesha kiwango bora na kadiri wanavyopata muda wa kucheza aanazidi kuimarika,” alisema Robertinho na aliongeza kuwa;

“Kadri siku zinavyozidi kwenda wachezaji wanazidi kuzoeana, mimi nimetoka Brazili nimecheza soka na sasa ni mwalimu mara zote naamini kwenye soka la kushambulia pamoja na kumiliki mchezo na hicho ndio nataka wachezaji wangu wakifanye,” alisema Robertinho.

Alisema anawapongeza wapinzani wao Dodoma jiji FC kwa kuonyesha soka nzuri na kuweza kuzuia mipango yao katika dakika 44 ya kipindi cha kwanza kabla ya kuruhusu bao la kwanza.

SOMA NA HII  OSCAR OSCAR AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA URAIS TFF