Home Habari za michezo LICHA YA UBUTU WA SAFU ZA USHAMBULIAJI YANGA, GAMONDI AFUNGUKA SOKA LAKE...

LICHA YA UBUTU WA SAFU ZA USHAMBULIAJI YANGA, GAMONDI AFUNGUKA SOKA LAKE HILI

Habari za Yanga leo

Kocha Miguel Gamondi alisema licha ya ubutu wa safu ya ushambuliaji ila hana wasiwasi na hilo kutokana na aina ya soka analofundisha kwani kila mchezaji anatakiwa kufunga bila kujali nafasi anayoicheza.

“Soka ninalofundisha ni la kushambulia na kukaba hivyo kila mchezaji uwanjani anatakiwa kufanya kazi bila kumwangalia nani anatakiwa kufanya nini, washambuliaji pia wanatakiwa kusaidia kukaba pale inapohitajika;

“Sifurahishwi na idadi ndogo ya mabao kutokana na nafasi nyingi zinazotengenezwa lakini hili halinifanyi kuamini kikosi changu kina mapungufu kwa sababu kwenye mechi nne imefunga mabao matano ambao sio wastani mbaya.”

SOMA NA HII  LEO NDO LEO SIKU YA KUTUSUA MKWANJA NA MERIDIANBET ....ODDS ZA USHINDI HIZI HAPA...