Home Habari za michezo UKATILI WA CHA MALONE KWA YANGA JANA WAMUIBUA DEWJI….ALICHOKISEMA HIKI HAPA…

UKATILI WA CHA MALONE KWA YANGA JANA WAMUIBUA DEWJI….ALICHOKISEMA HIKI HAPA…

Habari za Simba

MFADHILI wa zamani wa Simba, Azim Dewji amemuangalia beki mpya, Che Malone Fondoh kisha akajikuta anafurahia tu kazi yake akidai jamaa ni beki wa maana sana,

Dewji alisema Che Malone ni beki wa kisasa ambaye uchezaji wake eneo la ulinzi anatumia akili nyingi na nguvu kiasi kuwadhibiti washambuliaji.

Dewji alisema beki huyo akicheza sambamba na Henock Inonga haoni kama itakuwa rahisi kwa timu hiyo kufungwa magoli ya kizembe

“Tuna ukuta mzuri nimefarijika sana kuona jinsi mabeki wetu wa kati wanavyocheza, kama yule beki mpya wa Cameroon (Che Malone) ni beki mwenye hesabu nzuri sana hana mapepe wala sio mtu wa kutumia nguvu sana,” alisema Dewji ambaye wakati Simba ikicheza fainali ya CAF mwaka 1993 ilikuwa chini ya ufadhili wake.

“Tumepata beki mzuri sana nawapongeza viongozi, kwa uchezaji wa beki yule ukichanganya na hawa wenzake aliowakuta napata imani kwamba washambuliaji wa timu zingine kazi wanayo.

SOMA NA HII  WAKATI JANA WAKIPOTEZA KOMBE LA CAF.....RAIS WA FIFA ATOA NENO YANGA...TFF WATAJWA...