Home Habari za michezo UNAAMBIWA MTIBWA SUGAR WAAMKA NA SIMBA SC…. ISHU IKO HIVI

UNAAMBIWA MTIBWA SUGAR WAAMKA NA SIMBA SC…. ISHU IKO HIVI

Timu ya Mtibwa Sugar kutoka Morogoro, imetamba kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/24 dhidi ya Simba SC ya Dar es salaam.

Mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, utapigwa Alhamis (Agosti 17), huu kwenye Uwanja wa Manungu uliopo Turiani mkoani Morogoro.

Afisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, amewataka wapinzani wao hao kujiandaa kisaikolojia na mchezo huo kwani matokeo watakayoyapata hawatayaamini.

Kifaru ameongeza kuwa, anafahamu mchezo huo utakuwa mgumu kwani Simba SC watataka kupata ushindi, lakini na wao wamejiandaa vizuri, hivyo watahakikisha wanaibuka na alama zote tatu.

“Tunawaambia hao Simba SC wasitarajie mteremko kutoka kwetu kwenye mchezo huo, ule unyonge tuliouonesha msimu uliopita hautotokea msimu huu, kwa sasa tupo ngangari,” amesema Kifaru.

SOMA NA HII  SIMBA WAPATA PIGO.... KRAMO MAMBO SIO MAMBO, DAKTARI AANIKA UKWELI WOTE