Home Habari za michezo WAKATI ‘SKUDU’ AKIRUDI ….TFF NAO WAANZA KUFANYA YAO KWA YANGA….

WAKATI ‘SKUDU’ AKIRUDI ….TFF NAO WAANZA KUFANYA YAO KWA YANGA….

habari za yanga

Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Mahlatsi Makudubela ‘Skudu’, jana Jumanne (Agosti 15) alianza mazoezi na wenzie baada ya kupona majeraha aliyoyapata katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.

Skudu aliumia goti la mguu wa kushoto katika mchezo huo uliochezwa wiki iliyopita katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ambao Young Africans ilishinda mabao 2-0.

Nyota huyo raia wa Afrika Kusini alitolewa uwanjani dakika ya sita ya mchezo huo baada ya kuchezewa rafu na James Akamiko na nafasi yake kuchukuliwa na Chrispin Ngushi.

Daktari wa Young Africans, Moses Etutu, amesema Skudu alipatwa na maumivu makali hali ambayo walilazimika kwenda hospitali baada mchezo kumalizika.

Amesema walimpeleka hospitali mchezaji huyo na kufanyiwa vipimo lakini bahati nzuri alionekana hajavunjika hivyo wakaruhusiwa kurudi naye kambini.

“Kwa sasa anaendelea vizuri, leo (jana) ataanza mazoezi na wenzake baada ya kumaliza programu yake pekee yake na kuinekana yupo fiti,” amesema.

Staa huyo ambaye anatumia mguu wa kushoto, anasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu hiyo ambao wanaamini atakuwa msaada mkubwa katika kikosi cha timu hiyo katika msimu wa 2023/2024.

Skudu aliyejiunga na Young Africans kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Marumo Galants ya Afrika Kusini, amewahi kupita katika klabu za Orlando Pirates, Chippa United, Platinum Stars na nyingine.

RATIBA YAPANGULIWA MAPEMA TU…

Aidha katika hatua nyingine Klabu ya Yanga SC ilipaswa kucheza mchezo wa kwanza wa NBC Premier League dhidi ya KMC katika Dimba la Azam Complex Chamazi kesho Agosti 17, 2023.

Kutokana na ushiriki wa Yanga Sc katika mashindamo ya kimataifa, hivyo mchezo huo umesogezwa mbele na utachezwa Agosti 23, badala ya Agosti 17 kama ilivyopangwa hapo awali.

Hivyo KMC atacheza dhidi ya Namungo FC Katika Dimba la Ruangwa Lindi tarehe 19, Agosti wakiwasubiri Yanga SC kucheza mchezo wao wa Kimataifa dhidi ya ASAS FC ya Djibouti, Agosti 20, 2023.

SOMA NA HII  BAADA YA KUCHAPWA JUZI...KOCHA MAN UTD AJA NA STAILI MPYA YA KUJITETEA...AWASHUSHIA LAWAMA MASTAA ...